Mzee miaka 90 mbaroni kwa kubaka wanafunzi wa tano...soma habari kamili na matukii360...#share


Na Mwandishi Wetu, Shinyanga


JESHI la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mzee Kachuka Malongo (90), kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi watano wa shule ya msingi kwa nyakati tofauti.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule amesema kwamba wanafunzi hao ni wenye umri wa miaka minane hadi 12, na alikuwa akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa, kutokana na uchu wa mapenzi aliokuwa nao.

“Tumebaini chanzo cha tukio hilo kuwa ni tamaa na uchu wa mapenzi, kwa hiyo tunamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani”, amesema Kamanda Haule.

Kamanda Haule aliendelea kwa kusema kwamba taarifa za watoto hao kufanyiwa vitendo hivyo vya ukatili walizipata kwa mkazi wa eneo hilo Amada Mganyizi, na ndipo walipoamua kuzifuatilia na kumkamata mtuhumiwa.

Pia Kamanda Haule amewataka wazai kuwa makini na karibu na watoto wao, ili kubaini matatizo yao au jambo lolote linapowatokea.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search