Magufuli kuapisha mabalozi...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS John Magufuli kesho atawaapisha mabalozi wateule wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Rwanda na Urusi.
Rais John Magufuli
Kwa mujibu wa taarifa ya katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi iliyotolewa leo imeeleza rais Magufuli atawaapisha IGP-Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda na Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.





No comments:
Post a Comment