Serikali: Wanafunzi wapime TB kabla kuingia shule...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu, amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na shule za bweni bila kupima
ugonjwa wa kifua kikuu (TB).
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa amemgeukia mmoja wa watoto mwenye tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu akiwa anakunya dawa iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.
Amepiga marufuku hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wadau wa afya katika uzinduzi wa dawa ya watoto ya ugonjwa huo (New TB Paediatric Formulation) pamoja
na kukabidhi mashine tano (Genexpert Machines) kwa hspitali binafsi kwa ajili
ya kusaidia kutoa hudua ya vipimo vya ugonjwa huo.
“Hakuna mwanafunzi ataingia katika shule ya bweni bila
kupimwa ugonjwa wa kifua kikuu, narudia kutoa maelekezo kwa waganga wafawidhi
zile fomu za afya wanatakiwa wafanye uchunguzi na siyo kutia saini tu, nakusema
tumemuangalia yuko sawa, tutawaua watoto wetu kama hatutachukua hatua ya
kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu,” amesema Ummy.
Waziri Ummy amesema kwa mujibu wa makadirio ya mwaka 2016
watu takribani laki 160,000 huwa na matatizo ya ugonjwa wa kifua kikuu nchini
kila mwaka ambapo kati ya hao watoto ni 6457.
Amefafanua kuwa katia ya wagonjwa hao laki 160,000 ni watu
takribani 65900 tu ambao waliweza kufikiwa na kuwekwa kwenye mpango wa
matibabu.
Amesema TB ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa
kusababisha vifo vingi, kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) mwaka 2016
takribani watu milioni 1.3 walifariki dunia kutokana na ugonjwa huo.
“Na hapa nchini kwetu kwa takwimu ambazo tunazo zinaonesha
kwamba jumla ya vifo vinavyotokea miongoni mwa hao ambao wanamatatizo ya kifua
kikuu kwa mwaka ni vifo 28000 sawa na vifo 77 kila siku,” amesema.
Amiongeza kwamba kwa mujibu wa takwimu pia za WHO inakadiriwa
kuwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua ugonjwa huo kila mwaka ambapo milioni 1
kati ya hao ni wa toto wa chini ya umri wa miaka 14.
Amesema asilimia 90 ya watu 100 wanaokwenda hospitali na
kupata matibabu , watu 90 wanapona kabisa hivyo changamoto ni jinsi ya kuwapata
wagonjwa ncnini na kuweza kuwaingiza kwenye mfumo wa matibabu.
Akitaja hospitali zilizokabidhiwa mashine hizo kwa ajili ya
kufanya vipimo na kuibua wagonjwa wapya ni Aga Khan, Kairuki, Regency, TMJ na
Shree Hindu Mandal.




No comments:
Post a Comment