Majaliwa ampa mlemavu milioni tano.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu,Dar es salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemkabidhi Bibi Tecla Hamidu ambaye ni mlemavu wa miguu sh. milioni tano ili aweze kuongezea katika mtaji wake.
Kassim Majaliwa alizungumza katika Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes).

Ametoa fedha hizo leo (Jumanne, Machi 20, 2018) jijini Dar es salaam ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa Februari 22, 2018 kwenye Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes).

Waziri Mkuu alitoa ahadi hiyo baada ya Bibi Tecla ambaye ni mjasiriamali anayejihusisha na ushonaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo kumuomba amchangie sh. 500,000 ili aweze kuongezea mtaji wake.

Wakati akimkabidhi fedha hizo, Waziri Mkuu amesema kwamba anatarajia zitamsaidia katika kuongeza  mtaji wake, hivyo atazalisha bidhaa nyingi zenye ubora unaohitajika katika masoko ya ndani na nje.

Kwa upande wake, Bibi Tecla alimshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo na ameahidi kuzitumia fedha hizo kama ilivyo kusudiwa.

“Nashukuru kwa msaada huu kwani kuna watu wanakopa sh. laki mbili ili waongeze mitaji, lakini mimi leo nimepewa milioni tano bure na kiongozi wetu,”

Amesema licha ya kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa masoko anaamini tatizo hilo litakuwa historia baada ya kuwa na mtaji wa kutosha kwani atakwenda kuzalisha bidhaa zenye ubora zaidi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search