Faru wa kipekee aliyekuwa amesalia duniani afariki...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
 FARU pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na miaka 45, shirika la Ol Pejeta limetangaza.
Faru huyo alikuwa akitibiwa nchini Sudan katika shamba kubwa la kuhifadhi  wanyama la kituo hicho kwa muda kutokana na matatizo yaliyotokana na kuzeeka kwake 
Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na umri wake.

Shirika la Ol Pejeta limesema hali yake ilidhoofika sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
"Hakuweza hata kusimama na alikuwa anateseka sana," Ol Pejeta wamesema kupitia taarifa.
Alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya kuangamia.
Alinusurika kuuawa porini alipohamishiwa katika kituo cha kuhifadhi wanyama cha Dvur Kralove nchini Jamhuri ya Czech miaka ya 1970.
Mwaka 2009, alirejeshwa Afrika na kuanza kutunzwa katika kituo cha Ol Pejeta katika jimbo la Laikipia.
Alichangia kuendeleza faru wa aina yake kwa kutungisha mimba faru wengine na kuchangia kuzaliwa kwa faru wengine wawili wa aina yake ambao sasa ndio pekee waliosalia hai.
Faru hao kwa jina Najin na Fatu ni wa kike lakini ni tasa.
"Kadhalika, chembe za jeni zake zilichukuliwa na kuhifadhiwa jana kabla ya kifo chake kwa matumaini kwamba zitasaidia katika juhudi za siku za usoni za kuwazalisha faru kupitia teknolojia ya jeni na seli," Ol Pejeta wamesema.
Matumaini pekee sasa ya kuendeleza faru wa aina ya Northern White Rhino ni kupitia teknolojia ya kutungisha mbegu kwenye mayai ya mnyama nje ya mwili wa mnyama huyo, maarufu kama IVF.
Hilo linatarajiwa kufanyika kwa kutumia mayai yaliyovunwa kutoka kwa faru jike walio hai kwa sasa pamoja na mbegu za kiume kutoka kwa faru wengine wa kaskazini.
Shughuli ya kutungisha mbegu mayai hayo ikifanikiwa, basi faru wa karibu aina ya Southern White Rhino watatumiwa kubeba mimba hiyo.

Mwaka uliopita, shirika la Ol Pejeta lilizindua kampeni ya kuchangisha pesa kupitia kufungua akaunti kwenye mtandao wa kutafuta wapenzi wa Tinder
Lengo lilikuwa kuchangisha dola milioni 9 zitakazofadhili utafiti wa kutafuta mbinu mbadala za kutumia mbegu zao kuzalisha.
Tinder inaongoza ulimwenguni miongoni mwa mitandao ya kijamii inayotumika kutafuta marafiki na wapenzi.
Kupitia kampeni #TheMostEligibleBachelor, Tinder walitumai picha ya Sudan ingeonekana katika mataifa 190 ulimwenguni.
Kampeni hiyo ilidhaniwa kuwa njia pekee iliyosalia ya kuokoa faru hao wanaokabiliwa na hatari kubwa ya kuangamia.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search