Majaliwa: Wafanyabiashara tumieni taasisi za kifedha kukopa...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Ruangwa
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara wilayani Ruangwa kutumia taasisi
za kifedha kukopa fedha kwa ajili ya kukuza mitaji yao.
Kassim Majaliwa
Ameyasema hayo leo (Jumapili,
Machi 25, 2018) wakati akizungumza na wafanyabiashara wa wilaya hiyo katika
kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama Cha Walimu, wilayani Ruangwa.
Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani
Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ni vema wakatumia taasisi za
kifedha zilizopo ili kukuza mitaji yao.
”Naamini sekta ya biashara ni
muhimu katika mabadiliko ya maendeleo, hivyo wafanyabiashara ni chachu ya
maendeleo kokote na Serikali itaendelea kuwaunga mkono.”
Amesema katika kuhakikisha riba
zinapungua, Rais John Magufuli anaendelea kuzungumza na wamiliki wa taasisi za
kifedha ili waone namna ya kupunguza riba hiyo.
Waziri Mkuu amesema lengo la
Serikali la kuchukua hatua hiyo ni katika kutekeleza mkakati wake wa
kuwawezesha wafanyabiashara ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu.
Pia Waziri Mkuu amewahakikishia
wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali ipo pamoja nao na imedhamilia kuboresha
huduma mbalimbali za jamii kama maji na afya.
Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wafanyabiashara wa Wilaya ya Ruangwa, Said Shea amewaomba wafanyabiashara
wenzake watumie fursa za maendeleo zilizoko wilayani humo kwa kupanua wigo wa
biashara zao.
No comments:
Post a Comment