Warami watoa ya mayoni kwa maaskofu...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaama
WATETEZI wa Rasilimali Wasio na Mipaka (Warami) wemeshauri Maaskofu kujikita kwenye masuala mahususi yanayohusu
dini katika kuelimisha na kumuachia kaisali yaliyo yake na ya Mungu yaliyo
yake.
Mkurugenzi wa Utafiti Warami Philipo Mwakibinga, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Ushauri huo umekuja
siku moja baada ya kusambaa kwa ujumbe wa pasaka kutoka baraza la maaskofu wa Kanisa
la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kusainiwa
na maaskofu 27 ukizungumzia masuala mbalimbali ya kijamii, kisiasa, kiuchumi kwa
kukosoa na kushauri huku ukiitaka serikali kuchukua hatua hususani suala la
katiba mpya.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Utafiti Warami
Philipo Mwakibinga, amesema viongozi wa dini wana wajibu wa kiutumishi katika
jamii huku wakilinda dhamira yao ya kuhakikisha umoja wa nchi unabaki kuwa
salama kwa namna yoyote ile.
“Jana tuliona katika
mitandao ya kijamii waraka wa viongozi wetu wa dini, ukizungumzia masuala mbali
mbali ya nchi na mwelekeo wake huku sehemu kubwa ya waraka huo ukijikita katika
kuikosoa serikali juu ya namna inavyoendeshwa,” amesema Mwakibinga.
Ameongeza “Tunatoa wito
kwa Maaskofu wetu kujikita katika masuala mahususi yanayohusu dini,
watuelimishe kwenye dini, wamuachie kaisari yaliyo yake na ya Mungu yaliyo
yake,”
Amedai kushangaa waraka
huo wa salamu za Pasaka kutojikita zaidi katika kuwasisitiza waumini wake
kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, Kusoma biblia na maandiko mengine
ya dini na badala yake wakajikita katika
maoni yanayong’ata na kupuliza.
Mwakibinga amesema
kwamba kwa sasa nchi imejitanabaisha katika kutatua changamoto zilizokuwa
zinasemwa kila siku na wanasiasa hasa wa upinzani ambapo matunda yameanza
kuonekana kwa sasa kwani serikali inazishughulikia.
Amewaomba maaskofu
kuchagua njia sahihi ya kupita kama walivyofanya wenzao waliowatangulia kwani
kuna viongozi wa dini walipoona wanawito wa kushiriki siasa waliamua kuachana
na upadri na uaskofu na kujikita kwenye siasa.
No comments:
Post a Comment