Mtanange Simba Vs Yanga Aprili 29.....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo,  Boniface Wambura leo imetangaza rasmi tarehe ambayo Watani wa Jadi (Simba SC na Yanga SC)  zitacheza mchezo wa pili wa marudiano wa ligi kuu ya soka Tanzania bara (VPL)
Boniface Wambura

Pamoja na mechi nyingine ambazo leo zimetolewa ratiba yake rasmi, Wambura alitangaza rasmi sasa mtanange wa watani hao utafanyika Aprili 29, 2018 jijini Dar es salaam katika uwanja wa taifa.

Ratiba kamili;
Aprili 3;   Njombe Mji FC Vs Simba
Aprili  9;  Mtibwa vs Simba 
Aprili 20; Lipuli FC vs Simba 
Aprili 29; Simba vs Yanga 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search