Tetesi za soka Ulaya leo Jumatatu...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Everton wanataka Arsene Wenger kuwa meneja wao ikiwa atafutwa na Arsenal. Mmliki wa klabu ya Everton Farhad Moshiri anaamini kuwa Wenger ni bora zaidi kuisaidia Everton kujijenga. (Star)
Asernal Wenger
Meneja mjerumani Joachim Low anaibuka kama mtu anayeweza kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Mail on Sunday)
Chelsea wana mpango wa kumleta mchezaji wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta katika safu yake ya usimamizi. (Mirror)
Arsenal wanataka mrithi wa Wenger kuwa kocha mkuu badala ya meneja, hatua ambayo itampa fursa zaidi ya kufunza.(Sun)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry, anasema atakubanli ikiwa ataombwa kuchukua mahala pake Arsen Wenger. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain, anasema lawama dhidi yake kwa kuhamia Anfield kutoka Arsenal ni upuuzi akisema kuwa lawama hizo hazina athari yoyote kwake.(Mirror)
Mshambuliaji wa Brazil Willian, 29, anasema anataka kusalia katika klabu hiyo ya Premier League licha Manchester United kuonyesha nia ya kumsaini (Planeta Sportv - in Portuguese)
Tottenham wanamtaka mchezaji wa Bayer Leverkusen mlinzi raia wa Ujerumani Jonathan Tah, 22 kuchukua mahala pake Toby Alderweireld. Tottenham wameshindwa kuafikiana mkataba mpya na mchezaji huyo wa miaka 29. (Mirror)
Paris Saint-Germain hawatamuuza Neymar mwisho wa msimu, kwa mujibu wa mkurugenzi Antero Henrique, licha ya mchezaji huyo wa miaka 26 kuhusishwa na Real Madrid. (Goal via L'Equipe)
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema haelewi vizuri kuhusu kikosi watakachokutana nacho Jumatatu usiku cha Manchester United. (Sun)
West Brom wanajiandaa na kuondoka kwa wachezaji wengi ikiwa watashuka katika jedwali ambapo mlinzi wa Northern Ireland Jonny Evans, 30, kipa wa England Ben Foster, 34, mlinzi wa England Craig Dawson, 27, na msambulizi wa England Jay Rodriguez, 28, ambao wote wanavutia vilabu vingine. (Sun on Sunday)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search