Serikali:Kila kijiji kuwa na wahudumu wawili wa afya.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam

SERIKALI inatarajia kuweka wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika kila kijiji ili kuimarisha huduma ya afya ya msingi hasa kuwakinga wananchi ña magonjwa.



Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika majadiliano na wadau wa maendeleo, mashirika  yasiyo ya serikali,Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kila kijiji kitakuwa na watoa huduma wawili.

"Kazi yao kubwa si kutibu bali kuhimiza masuala ya lishe, kuhimiza masuala ya uzazi wa mpango, watu kujua hali zao kama wanamaambukizi au la na pia kuwaelekeza wapi waende kupata huduma za afya, "amesema.

Amesema ifikapo 2020 matarajio ni wahudumu wa afya zaidi ya 30,000  katika vijiji 15,000 nchini.

Amesema tayari wadau hao wa maendeleo wamekubali kushirikiana ña serikali ambapo watatoa elimu kwa watoa huduma hao kwani ni muhimu na litaonesha matokeo ya haraka.

Mkurugenzi wa Programu Taasisi ya Benjamini Mkapa,Rahel Sheiza amesema kuna haja ya kuwa na uwiano katika uwekezaji wa vituo vya kutolea huduma na ngazi ya jamii.

Mratibu wa huduma ya jamii kutoka Wizara ya Afya, Dk Anna Kisangala amesema mkakati ni kukinga zaidi kuliko kutibu.

"Mhudumu wa afya akiwa kwenye jamii anaweza kutambua watu waliopo kwenye matatizo," amesema

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search