Utelezi, kona kali chanzo ajali ya treni....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Kigoma
TAARIFA za awali zimeeleza utelezi na kona kali ndio chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora.
Takriban watu 29 wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea jana mchana eneo la kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka.
Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela ameambia matukio360 kuwa; "Sababu za awali za ajali hiyo kupitia timu yetu ya kutathmini ajali ni utelezi na kona kali," amesema.
Ajali ilitokea majira ya saa saba na dakika hamsini mchana eneo la katikati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza.
"Tathmini kamili ya ajali itatolewa pale ambapo mabehewa yatakuwa yameinuliwa."
Mapondela amesema eneo hilo si kwamba ni baya na halina historia ya kupata ajali yoyote ile.
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook kwamba amezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma na kufahamishwa kwamba chanzo cha ajali ni injini kupoteza njia kufuatia mchanga uliokuwa kwenye njia ya reli. "Naomba uchunguzi ufanyike ili kuona kama mchanga ule ni sababu ya mvua kubwa zinazonyesha ama la. Treni ndio usafiri wa wanyonge wengi mkoani kwetu hivyo ajali za namna hii zinastusha na kuogopesha. Natoa pole sana kwa wana Kigoma na Watanzania wengine," amesema.

No comments:
Post a Comment