Tanesco yakanusha kuhusu LUKU....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii  inayodai kutakuwa na tatizo katika mfumo wa manunuzi ya LUKU kuanzia Machi 25 hadi Aprili 5 mwaka huu.

Taarifa hiyo inayodaiwa ya kutunga ilikuwa ikieleza kwamba kutokana na hali hiyo wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho.

Tanesco kupitia Ofisi ya Uhusiano imesema taarifa hizo si za kweli na uzushi wenye nia ya kupotosha umma kwani haijatokea taarifa yoyote kuhusu hitilafu katika mifumo ya manunuzi ya LUKU.

"Ikumbukwe kwamba taarifa kutoka Tanesco hazitolewi na mtu binafsi bali ofisi ya uhusiano iliyo chini idara ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo ni msimamizi wa utoaji taarifa za shirika hili,"imesema taarifa ya Tanesco.

Imewaomba wateja wote wa Tanesco waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote ."Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida."

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search