TTCL, Tigo kushirikiana katika huduma za kifedha...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

SHIRIKA la Mawasiliano nchini (TTCL) limeingia makubaliano ya ushirikiano wa biashara na kampuni  ya simu za mikononi ya Tigo yatakayowezesha wateja wa pande zote mbili kubadilishana fedha na huduma za kifedha kupitia simu zao za mkononi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuingia makubaliano hayo, Mkuu wa Huduma za TTCL-Pesa Moses Alphonce amesema kwa kushirikiana na Tigo katika huduma ya kifedha ya Tigo –Pesa utamwezesha mteja kutuma na kupokea fedha kwa gharama nafuu.

“Faida za ushirikiano huu, gharama ni nafuu unapotuma fedha kutoka Tigo-pesa kwenda TTCL-pesa, lakini vile vile unapotuma fedha kutoka TTCL-pesa kwenda Tigo-pesa,” amesema Alphonce.

Alphonce ameongeza kwamba kupitia ushirikiano huo utamrahisishia mteja kwani anapotuma au kutumiwa pesa itaingia moja kwa moja kwenye akaunti yake ambapo amebainisha kuwa lengo la TTCL-Pesa ni kuhakikisha kila mteja anafikiwa na huduma hiyo.

Amesema kutokana na huduma hii kufanyika kwa miamala ya simu, wamedhamiria kubadili mifumo ya malipo yote ya umma na binafsi ili yafanyike kupitia mtandao wa kidigitali na kuongeza usalama na ufanisi wa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake mkuu wa huduma za Tigo pesa Hussein Sayed, amesema kuwa Tigo pesa imeazimia kufikisha huduma sehemu mbalimbali ambazo huduma za kifedha hazijafika ili kuwawezesha wateja kufanya huduma za kifedha  kutoka Tigo-Pesa  kwenda TTCL-Pesa kwa kiwango kilekile.

Hata hivyo hatua hii ya makubaliano kati ya TTCL na Tigo ni muendelezo wa jitihada za shirika la mawasiliano nchini kurejesha soko la huduma za mawasiliano nchini  kwani hadi sasa TTCL imefanikiwa kufikisha huduma za 4G lite kutoka mikoa 16 ya Tanzania bara na Visiwa vya Pemba na Unguja.

Mkuu wa Kitengo cha TTCL Pesa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Moses Alphonce (kulia) na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Fedha Tigo Hussein Sayed wakipongezana kama ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma za kifedha kwa jia ya mtandao katika ya TTCL Pesa na Tigo Pesa hafla hiyo imefanyika kwenye Ukumbi Golden Jubilee Tower (PSPF) jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha TTCL Pesa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL)  Moses Alphonce (kulia) na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Fedha Tigo Hussein Sayed wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzao wa TTCL na Tigo mara baada ya uzinduzi huo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search