Dk. Rwakatare atunukiwa tuzo ya heshima...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
MCHUNGAJI Kiongozi wa
Kanisa la Mlima wa Moto la Assemlies of God Mikocheni B jijini Dar es Salaam
Dk. Getrude Rwakatare ametunukiwa tuzo ya heshima na Shirika la Umoja wa
Maaskofu na Wachungaji ulimwenguni.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto la Assemlies of God Mikocheni B jijini Dar es Salaam Dk. Getrude Rwakatare akiwa ameshika tuzo aliyokabidhiwa.
Tuzo hiyo imetolewa na
Rais wa umoja huo Askofu Mkuu Steve Moore kutoka Washington D.C nchini Marekani
na kukabidhiwa na Askofu Mkuu Professa Leonard Kuwas mwakilishi wa Afrika.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Dk.
Rwakatare amesema tuzo hiyo ameipata kutokana na utumishi wake bora kiroho na
kijamii nchini.
“Leo ninayo furaha ya
kipekee kwa kutunukiwa tuzo ya heshima kutokana na utumishi bora kiroho na
kijamii katika nchi yangu ya Tanzania,” amesema Dk. Rwakatare.
“Tuzo hii imetokana na
watu hawa kunifuatilia kwa miaka yote ya utumishi wangu tangu nikisomea uchungaji nchini Marekani na niliporudi
niliendelea kufanya shughuli za kiutumishi na kijamii,” ameongeza.
Dk. Rwakatare amesema
katika kuhakikisha anatoa utumishi wa kiroho
na kijamii aliweza kuanzisha kanisa ambalo limeweza kuenea kwenye maeneo
mbalimbali nchini pamoja na kuanzisha shule kwa ajili ya kuhudumia watoto
kwenye masuala ya elimu.
Aidha amesema aliweza
kuwasaidia akina mama katika masuala ya mikopo, misaada mbalimbali katika jamii
na kuwasaidia wengine kuwainua kwa njia ya maombi.
Kwa kupata tuzo hiyo
Dk. Rwakatare anakuwa mtu wa kwanza kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kutunukiwa.
“Ninayo furaha ya
kusema kuwa mimi ni wa kwanza kupewa tuzo hii, kwa hiyo nina mshukuru Mungu,”
amesema.
Aidha kwa kuchukua tuzo
hiyo amechaguliwa kuwa mmoja wa sehemu ya kamati kuu ya ulimwengu mzima katika
umoja huo.
Ameahidi kutumikia
nafasi hiyo kwa uaminifu na atakuwa katika maombi kuombea viongozi wote.
Matukio katika picha.
No comments:
Post a Comment