Kesi ya Mbowe na Wenzake kusikilizwa Aprili 16, 2018...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe Aprili 16, 2018.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa hakimu Wilbard Mashauri baada ya kukubaliana  na mapendekezo ya upande wa utetezi kufanyika kwa usikilizwaji wa awali.

Awali upande wa mashtaka katika kesi hiyo uliiomba Mahakama hiyo kuruhusu kesi  isikilizwe kwa haraka, ikiwezekana kuanza kesho.

Wakili huyo wa Serikali, Faraja Nchimbi  alisema msingi wa  maombi hayo ni kutokana na upelelezi kukamilika.

Alisesema sababu nyingine ni kwamba washtakiwa wengi katika kesi hiyo ni wabunge na kwa kuwa kesi hiyo inavuta watu wengi ni vema ikasikilizwa haraka.

"Kwa hiyo tunaomba kama ikiwezekana kesho mchana tuendelee na usikilizaji wa awali ili sisi upande wa mashtaka tuweze kuwasilisha kile tulicho nacho,” amesema Nchimbi.

Hata hivyo, wakili wa upande wa utetezi,  Peter Kibatala alipinga mapendekezo hayo akieleza kuwa ndiyo kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, kesho atakuwa na kesi nyingine Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na kesho kutwa pia atakuwa na kesi nyingine.

Alisema Aprili watakuwa na semina za mawakili ambazo ni za lazima kwa kuwa bila kupata alama zinazohitajika kutokana na semina hizo, leseni yake haiwezi kuhuishwa.

Vilevile, alisema kuanzia Aprili 13 watakuwa na mkutano wa mawakili wote jijini  Arusha na akapendekeza usikilizwaji wa awali  wa kesi hiyo ufanyike Aprili 16.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe hiyo, itakapoitwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.

Mbali ya Mbowe viongozi wengine walioachiwa kwa dhamana ni Katibu Mkuu Dk  Vicent Mashinji, Manaibu Katibu Wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa,  Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho Ester Matiku  na mwenyekiti wa baraza hilo, Halima Mdee.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search