Magufuli ateua katibu tawala Tabora...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS John Pombe Magufuli amemteua Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Makungu anachukua nafasi ya Dk. Thea Ntara ambaye amestaafu.
Uteuzi wa Makungu unaanzia tarehe 20 Aprili, 2018 na tarehe ya kuapishwa kwake itapangwa baadaye.
No comments:
Post a Comment