Mdachi: Vijana changamkieni fursa za mafunzo zinazotolewa na chuo cha NCT...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
VIJANA nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za mafunzo
yanayotolewa na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) ili kuwawezesha kutapa ujuzi utakaowasaidia kuwapa ajira
pamoja na kujiajiri wenyewe.
Mkurugenzi mkuu wa
bodi ya utalii Tanzania. Devotha Mdachi akiongea wakati wa ufunguzi wa tamasha la maonyesho ya la taaluma katika chuo cha taifa
cha utalii (NCT), jijini Dar Es Salaam
Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu
wa Bodi ya chuo hicho Devotha Mdachi alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi
wa tamasha la maonyesho ya taaluma
chuoni hapo.
“Vijana jitokezeni kuchangamkia fursa zinazotolewa na chuo hiki,
zitawasaidia katika kutatua tatizo la
ukosefu wa ajira, sambamba na kuwaongeza kipato hivyo kuinua uchumi wa nchi”
alisema Mdachi.
Alisema serkali kupitia wizara ya maliasiri na utalii imetoa
gari moja dogo ambalo litawasaidia vijana katika kufanikisha utalii wa ndani
ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada
za chuo hicho katika kuendelea kutoa mafunzo yanayokidhi viwango vya kitaifa na
kimataifa.
Mwenyekiti
Wa Bodi Ya Ushauri ya Chuo cha Taifa cha Utalii Benadeta Nduguru akizungumza wakati wa
ufunguzi wa tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa
cha utalii (NCT), April 27 2018 jijini Dar Es Salaam.
Kwa upande wa Mwenyekiti Wa Bodi ya Ushauri ya NCT Benadeta
Nduguru, alisema wameandaa tamasha hilo lufatia kutambua umuhimu wa vijana
katika kujenga uchumi wa nchi sambamba na kuwakutanisha wadau kutoka taasisi
mbali mbali zinazojishughulisha na utoaji wa huduma za kupokea watalii,
mahoteli, waongoza watalii hili kuweza kujionea namna chuo hicho kinavyo toa
mafunzo yake.
Ndunguru aliongeza kuwa kupitia tamasha hilo wadau wataweza
kujionea jinsi chuo hicho kinavyoendesha shughuli zake hivyo kuwa moja ya njia
ya kuwawezesha wahitimu wao chuo hicho kupata ajira kwa urahisi.
Tamasha hilo lilibeba
ujumbe usemao "Fursa Za Ajira Kwa
Vijana Kupitia Taaluma Ya Ukarimu Na Utalii" ikiwa kama njia ya
kuufahamisha uuma juu ya mafunzo yatolewayo katika chuo cha taifa cha utalii.
Mkurugenzi wa chuo cha NCT Sporah Liana akifafanua jambo katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), jijini Dar Es Salaam.
Wadau kutoka taasisi mbali mbali wakiwasilisha mada katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), April 27 2018 jijini Dar Es Salaam.
Washiriki tamasha hilo kutoka taasisi mbalimbali wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), jijini Dar Es Salaam.
Mgeni rasmi katika tamasha la maonyesho ya taaluma Devotha Mdachi akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wakati alipotembelea mabanda ya wanafunzi hao kujionea namna shughuli zinazofanywa na kuratibiwa na chuo hicho katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), jijini Dar Es Salaam.
Washiriki wa tamasha hilo wakifatilia kwa makini mada ambazo zikiwasilishwa katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), jijini Dar Es Salaam.
Mgeni rasmi katika tamasha la maonyesho ya taaluma Devotha Mdachi akiwa katika picha ya pamoja na vingozi wa chuo icho pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika tamasha la maonyesho ya taaluma katika chuo cha taifa cha utalii (NCT), jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment