Mjema atoboa siri Ilala kufanya vizuri matokeo elimu ya msingi...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema ukaribu uliokuwepo baina ya
walimu na wazazi ndiyo sababu wilaya hiyo kufanya vizuri katika matokeo ya
mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi 2017.
Mjema amefichua siri hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa tuzo kwa
shule za msingi za wilaya hiyo zilizofanya vizuri katika matokeo hayo lengo
likiwa ni kutoa motisha kwa walimu pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ili
kuendelea kufanya vizuri zaidi.
“Halmashauri ya manispaa ya Ilala ilifanya vizuri katika matokeo ya
kumaliza elimu ya msingi, ilishika nafasi ya nne kimkoa na nafasi ya pili kiwilaya
hivyo tumeamua kutoa tuzo katika shule hizi ili iwe chachu ya kuongeza Ufaulu,”
amesema Mjema.

Amesema tuzo hizo zitawasaidia kuwakumbusha kufanya vizuri ili kufikia
nafasi ya kwanza kimkoa na kiwilaya.
Kwa upande wake Ofisa Elimu Msingi Elizabeth Thomas, amesema Idara ya
elimu ya Msingi imelenga kutoa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri katika matokeo
ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2017 zenye lengo la
kutoa motisha nakuwapongeza walimu kwa kazi kubwa ya ufundishaji na ujifinzaji
waliofanya na kuzaa matunda ya matokeo mazuri.
Amesema
Jumla ya shule 184, zikiwemo za Serikali 107 na zisizo za Serikali
77,ambapo jumla ya wanafunzi 21,704 walisajiliwa kufanya mtihani wakiwemo
wavulana 10,270 na wasichana 11,434.
Aidha
wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 21,569 wavulana 10,184 na wasichana
11,365 sawa na asilimia 99.3% waliofaulu ni wanafunzi 19,236 wakiwemo wavulana
9,199 na wasichana 10,037 sawa na asilimia 89% na wanafunzi wote hao wamechaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.
Amebainisha
kuwa tuzo hizo zimetolewa katika makundi mbalimbali zikiwemo shule kumi
bora,shule zilizopandisha ufaulu zaidi ukulinganishwa na ufaulu wa mwaka 2016,
kata iliyofanya vizuri, shule zilizofanya mtihani kwa Mara ya kwanza na
zikafanya vizuri pamoja na kutoa tuzo maalumu kwa wadau mbalimbali.







No comments:
Post a Comment