Nditiye aipongeza TPA...soma habari kamili na matukio360...#share

Naibu waziri wa ,ujenzi uchukuzi  na mawasiliano Mhandisi ATASHASTA NDITIYE ameipongeza mamlaka ya bandari Tanzania [TPA]

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

                Ikiwa ni miaka 13 ya utendaji kazi wa mamlaka ya bandari Tanzania TPA Imeelezwa kuwa tangu   Mamlaka hiyo  kuanzishawa miaka 13 iliyopita mizigo imekuwa ikiongezeka kwa nchi nzima kutoka tani milioni 8 mwaka 2005 hadi kufikia tani milioni 15 kufikia mwaka 2017 hali ambayo imeongeza maendeleo nchini.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha mamlaka hiyo na wadau mbali mbali kujadili miaka 13 tangu kuanzishwa kwake na hatma ya TPA kwa miaka ya baadaye na changamoto za kiutendaji katika mamlaka hiyo  Mhandisi ATASHASTA  NDITIYE amesema kuwa mamlaka hiyo imefanikiwa kuongeza mizigo kwa kiasi kikubwa katika bandari huku akiitolea mfano bandari ya Dar es salaam ambayo mizigo imeongezeka kwa asilimia 6.9 kutoka tani  milioni milioni 7 mwaka 2006 mpaka tani milioni 14 mwaka 2017.

Hata hivyo ameongeza kuwa serikali imeipatia TPA Dola za kimarekani milioni 400 ili kurekebisha kina cha bandari ya Dar es salaam ili iwe na eneo kubwa la kuhudumia meli za mizigo na lile la kugeukia meli.
Aidha kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari nchini TPA Mhandisi DEUSDEDIT KAKOKO  amesema kuwa mamlaka hiyo itahakikisha inaboresha huduma za uingizaji na utoaji mizigo bandarini kwa wakati kwa kuendelea kuboresha utendaji kazi wake na pia imekuwa ikitoa elimu kwa taasisi mbali mbali ambazo zimeitembelea mamlaka hiyo hasa katika kipindi hichi ambacho mamlaka hiyo inatimiza miaka 13 tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumzia uboreshaji wa huduma za mamlaka hiyo mkurugenzi huyo amesema kuwa,


‘’Tpa tutakuwa na  dirisha  la kielektroniki la kusaidia huduma za vibali vya uingizaji na utoaji wa mizigo bandarini hali ambayo itawasaidia wafanyabiashara kurahisisha shughuli zao kielektroniki na TPA ijayo itakuwa ni chachu ya mendeleo ya uchumi wa viwanda” amesema Mhandisi KAKOKO.

Mamlaka ya bandari Tanzania TPA ilianzishwa April 13 mwaka 2005 na inatarajia kutimiza miaka 13 tangu kuanzishwa kwake jumapili ya wiki hii.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search