Jalala awataka watanzania kuenzi amani na upendo nchini..soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATANZANIA wametakiwa kupendana kushirikiana na kushikamana bila kuangalia itikadi ya dini zao ili kuendelea kuenzi amani na upendo uliopo nchini kwa sasa.
Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam na Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia nchini Maulana Hemed Jalala, ikiwa leo maadhimisho ya siku ya Meraji duniani kote.
Jalala amesema kuwa siku ya Meraji ni siku ya kuhamasisha amani na upendo vilivyopotea katika nchi Palestina, kwani mitume wote walioishi katika ardhi hiyo walikuja kwa lengo moja la kuleta amani katika nchi hiyo na dunia kwa ujumla.
Ameendelea kusema kuwa siku ya Meraji ni siku ya mshikamano kwa watu wa dini zote ikiwemo Waislamu, Wakristo na Wayahudi kwa pamoja kuendelea kutetea na kulinda amani na mshikamano vilivyopotea ndani ya nchi ya Palestina.
Ameendelea kusema kuwa siku ya Meraji ni siku ya mshikamano kwa watu wa dini zote ikiwemo Waislamu, Wakristo na Wayahudi kwa pamoja kuendelea kutetea na kulinda amani na mshikamano vilivyopotea ndani ya nchi ya Palestina.
| Mkutano ukiendelea. |
Pamoja na hayo amesema kuwa nchi ya Palestina ni nchi ya kihistoria kwa kuwa mitume wengi waliotumwa na mungu waliishi hapo akiwemo Isaka, Yakubu Mtume Mohamad (S.A.W) na hata Ibrahimu Baba wa mataifa yote alizikwa katika ardhi hiyo.
“Lakini pia vitabu vinavyotumiwa na dini zote kubwa ikiwemo Injiri, Torati, Zaburi, na hata Quran vilishuka katika nchi hiyo na vinaimiza Amani Upendo na Ushirikiano, hivyo basi kama binadamu tunajukumu kubwa la kuhakikisha vitu hivyo wanavipata wananchi wanaoishi Palestina”. amesema Jalala.
Akiongea kwa upande wa Watanzania amesema kuwa Watanzania tukiwa na sifa ya kuwa kisiwa cha Amani tunapaswa kuilinda na kuitetea Amani yetu tusikubali Amani hii ikapotea kirahisi rahisi na tuzidi kuwaombea viongozi wetu watuongoze katika haki na usawa ili kuendelea kuilinda Amani yetu.
"katika kuangalia haya yote yanayotokea nchini ya Palestina kwa sasa sisi kama watanzania tunajifunza kwa namna gani tuilinde na kuitetea amani na yetu na tusikubali kuipoteza kwani ni Tunu tuliyopewa na Mwenyezi Mungu" alisisitiza Jalala



No comments:
Post a Comment