TECNO KUJA NA KAMERA YA AINA YAKE

Kufuatia matoleo ya simu mbalimbali yiliyotangulia, TECNO, imekua ikitajwa tajwa huku ikihusishwa na ujio wa toleo jipya ikikisiwa kuwa ni muendelezo wa matoleo ya Camon, ni ukweli usiopingika kuwa matoleo ya TECNO-Camon yamekua na kamera nzuri zaidi kufananishwa na matoleo mengine.

Miongoni mwa vivutizi vinavyoipa simu kipaumbele, bila shaka simu inatakiwa iwe na kamera yenye megapixel kubwa, TECNO, wamelizingatia hilo.

Baadhi ya kurasa za mitandaoni zimeihusisha kampuni ya TECNO juu ya ujio wa toleo jipya likipewa jina la Camon kufuatia histoia ya kampuni kuzindua Camon CX mwaka jana miezi kama hii, bado hakujawa na uhakika wa taaifa hizi hivyo ni propaganda tu.
Simu hiyo inakadiriwa kuwa na megapixel 16 mbele pamoja na flashi maalum kwa picha za ‘’selfie’’, uwezo wa kupiga picha zenye ubora wa HD, kamera yake ya nyuma kuja na megapixel nyingi zaidi ssambamba na flashi maalum zinaakisi mwanga ili kupata kuendana na mazingira.
Maswali kuhusiana na ujio wa simu hiyo `yamekua mengi sana pasina kupata majibu yenye uhakika, kamera inayoweza kupiga picha nyingi ndani ya mfupi zikiwa na ubora wa HD?, bado inaniacha na maswali yanayoamsha morali ya kutaka kujua zaidi.


Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti http//www.tecno-mobile.com.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search