Mahakama yapokea vielelezo kesi ya Nondo...soma habari kamili na matukio360...#share

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi, Iringa, imepokea vielelezo vya kimtandao vilivyoletwa na upande wa mashtaka dhidi ya Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Abdul Nondo.

Akizungumza Mahakamani hapo, leo Mei 10, Hakimu Mkazi, wa mahakama hiyo, John Mpitanjia amesema amepokea vielelezo hivyo baada ya kupitia sheria mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Mpitanjia amesema, mahakama inawajibu wa kupokea kila kielelezo kinachokuja mbele yake.

Baada ya uamuzi huo upande wa utetezi chini Wakili Chance Luoga uliridhia maamuzi hayo na kuomba kesi hiyo  iendelee tena Mei 14

Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu,(TSN) anakabiliwa  anakabiliwa na mashtaka mawili shtaka la kwanza ni kusambaza taarifa za uongo akiwa jijini Dar es Salaam kuwa ametekwa na kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search