Majaliwa aagiza wizara, mashirika na taasisi kutumia nishati mbadala...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza wizara, mashirika na
taasisi zote za Serikali na binafsi zianze kutumia nishati mbadala ili kuondoa
kabisa matumizi ya kuni na mkaa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua
wiki ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini hapa, ambapo amesisitiza
juu ya utunzaji wa mazingira
“Nitoe maagizo kwa wizara, ashirika na taasisi zote za serikali
na binafsi zianze kutumia nishati mbadala ili kuondoa kabisa matumizi ya kuni
na mkaa,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha amewataka wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira yao na
kujiepusha na tabia ya kukata miti hovyo, ikiwemo kutupa taka ngumu hovyo
katika maeneo yanayowazunguka.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kutunza mazingira na
kuwataka watanzania kutimiza wajibu huo.
“Kwa nzia sasa kila mtanzania anatakiwa kutumia mkaa mbadala, ili kuhifadhi misitu na
kupunguza uharibifu wa mazingira,” amesema.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira na
Muungano January
Makamba amesema lengo la
kuadhimisha siku hii ni kuhamasisha na kuelemisha wananchi kuhusu umuhimu wa
kutunza mazingira.
“Lengo la kuadhimisha siku hii ni kuhamasishana na kuelimishana
kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira, mwaka huu maadhimisho haya yanachukuliwa
kwa umuhimu mkubwa kutokana uharibifu mkubwa wa mazingira,” amesema Makamba.
Amesema pia lengo la kufanyia maadhimisho hayo jijini Dar es
Salaam kwa mwaka huu ni kutokana na jiji hilo kuwa kitivo cha uchumi wa nchi ambapo asilimia 70
ya mkaa wa kuni unatumika.
Waziri Makamba amesema Serikali ina mpango wa kupunguza matumizi
ya kuni na mkaa kutoka asilimia 50 hadi 36, na kwamba hiyo ndio faida ya
kutumia majiko ya vumbi la makaa ya mawe kwa kuhifadhi mazingira.
Nao baadhi ya wadau wa mazingira wameahidi kuendelea
kushirikiana na Serikali katika mapambano ya kulinda na kuhifadhi mazingira
Siku ya mazingira duniani kitaifa imeambatana na maonyesho
mbalimbali ya teknolojia ya uzalishaji
wa mkaa mbadala.
Matukio mbali mbali katika picha.
No comments:
Post a Comment