Serikali yaanza kutafuta mwekezaji mwingine mradi mabasi mwendokasi...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ili kupunguza tatizo la usafiri jijini Dar es Salaam, Serikali itawashirikisha Chama cha Wamiliki wa Daladala (UWADAR) ili kuwa miongoni mwa watoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart).

Akizungumza bungeni leo Mei 10,  Waziri Mkuu amesema wako wawekezaji wa ndani na nje wakiwamo Uwadar wenye uwezo wa kutoa huduma muhimu na Serikali inaendelea kuondoa changamoto zilizopo sasa na kupata mwekezaji mwingine atakayeingia magari na kuufanya usafiri huo kutoa huduma kwa ufanisi.

 Akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni(CCM) Maulid Mtulia, Majaliwa, amesema:

“Ni kweli tuna mradi wa usafirishaji wa Udart, muungano wa Uda na Dart, Serikali inajua miundombinu yetu hasa pale makao makuu ya mabasi (Jangwani), mgogoro wa undeshaji, sehemu yoyote kunapokuwa na muungano wa taasisi mbili kunakuwa na changamoto.”

Katika swali la msingi, Mtulia alitaka kujua mikakati ya Serikali kutatua mgogoro ulipo baina ya kampuni ya Udart na Maxmalipo jijini Dar es Salaam ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji hilo, Majaliwa amesema wanalifanyia kazi.

“Tunaingia awamu ya pili, tunaingia na mdau mwingine ili kuwa na ushindani zaidi,” amesema Majaliwa na kusisitiza kwamba ukiwa na mwendeshaji mmoja akipata tatizo mwingine anaendelea.

 Waziri Mkuu amesema iwapo itabainika mwendeshaji wa sasa akawa na matatizo  basi ataondolewa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search