Alichosema Nape baada ya Sugu kuachiwa huru...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemkaribisha uraini Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ baada ya kutoka gereza la Ruanda alipokuwa akitumikia kifungo chake .

Nape amesema kuwa anakumbuka Mbunge huyo ambaye pia ni msanii aliwahi kuimba juu yake wakat alipoanza siasa.

“Karibu tena Uraini brother!{nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo nilipoanza siasa},” ameandika Nape kupitia ukurasa wake Twitter.

Sugu na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya

Advertisement

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search