Upelelezi kesi kigogo TPA haujakamilika...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ,imeelezwa upelelezi wa kesi ya kujilimbikizia mali zenye thamani ya Sh.bilioni 1.4  zisizolingana na kipato chake halali inayomkabili Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,(TPA), Prosper Kimaro bado haujakamilika.

Taatifa hiyo imeelezwa leo mahakamani hapo na Wakili wa Serikali  Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ambapo  kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa.

Kutokana na taarifa hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 5 mwaka huu na kuutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi. Mshtakiwa huyo anashtakiwa  chini ya kifungu cha 27 (1)(4) cha sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Sh.1,178,370,334,  na magari  yenye thamani Sh 307,364,678.20, zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa ametenda kosa hilo kati ya mwaka 2012 na 2016.

Alidai mshtakiwa  akiwa maeneo ya Temeke  na mtumishi wa umma wa TPA kama Meneja wa Fedha, amekutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake halali cha zamani na  cha sasa.

Mali hizo ni nyumba mbili  zilizopo mtaa wa Uwazi Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 124.2,  kiwanja kilichopo Yombo Vituka chenye thamani ya Sh.milioni 12.9 . Nyumba   mbili  zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 63.5, nyumba tatu zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh.milioni  159.

 Nyumba nyingine tatu zenye thamani ya Sh.milioni  170.1,  nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.milioni   71.3.kiwanja  kilichopo Temeke chenye thamani ya Sh.milioni  35.Pia kiwanja chenye thamani ya Sh.milioni 25 na amejenga nyumba tatu ambazo zinathamani ya Sh.milioni  159 pamoja na  nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.milioni 106.Nyumba zenye thamani ya Sh.milioni  214,  nyumba  nne eneo la Viziwaziwa Kibaha Mjini zenye thamani ya Sh.milioni 199.7 na nyumba nyingine iliyopo Kilimahewa Tandika yenye thamani ya Sh.milioni 70.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa pia anamiliki magari aina ya Toyota Land cruise lenye thamani ya Sh.milioni 180.1,  Mitsubishi lenye thamani ya Sh.milioni 38.4,  Massey Ferguson lenye thamani ya Sh.milioni  24 na Trailer lenye thamani ya Sh.milioni  4.5.

Mengine ni  Toyota Harrier yenye thamani ya Sh.milioni  35.8,  Trailer lenye thamani ya Sh.milioni 4.8,  na Massey Ferguson lenye lenye thamani ya Sh.milioni 19.1.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa  huyo alikana shtaka  na yupo nje kwa dhamana. Hiyo ni baada ya kukamilisha masharti ya  kuwa na wadhamini wawili ambao kila mdhamini  awasilishe hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh.milioni 200.

Pia alimtaka mshtakiwa huyo  asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama na mshtakiwa awasilishe hati zake za kisafiria mahakamani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search