Magufuli amefanya uteuzi mwingine... soma habari kamili na matukio360...#share

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Prof Andrew Barnabas Pembe kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa Prof. Pembe umeanza siku ya leo.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Pembe alikuwa Mhadhiri  na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search