Makamba: Tuna mkakati wa kuzunguka nchi nzima kuelimisha utunzaji wa Mazingira...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Januari Makamba amesema Serikali  inamkakati wa kufanya kampeni  nchi nzima ya kutoa elimu  ya utunzaji wa mazingira na athari zake kwa wazalishaji  na watumiaji wa mkaa.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tamasha la kuelimusha wananchi juu ya utunzaji wa Mazingira lililofanyika Mbagala halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya maadhimisho ya Mazingira.

"Hatutaishia tu hapa, tunamkakati wa kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kuelimisha wananchi kutunza mazingira hususani kwa kutumia nishati mbadala ya mkaa na kuni, " amesema Makamba.

Makamba amesisitiza kwamba katika kampeni hiyo watawahimiza watumiaji wa mkaa kutumia nishati mbadala ambazo zipo sokoni na huku wazalishaji wa mkaa watahimizwa na kuwatafutia namna nyingine ya kipato badala ya kukata miti.

Amesema mkoa wa Tabora unaongoza kwa kuzalisha mkaa, pamoja  mikoa mingi kutumia mkaa huku  mkoa wa Dar es salaam ukitumia mkaa kwa  asilimia 70 katika mikoa yote inayotumia mkaa.

Akizungumza na wananchi katika tamasha hilo amewataka kutunza mazingira kwa ajili ya vizazi vya sais na vya baadae ambapo amesema kila mtu anawajibu wa kutunza Mazingira.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya temeke Felix Lyaviva akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewahimiza wananchi kupanda miti ya matunda kwa faida yao na taifa kwa ujumla huku akisisitiza juu ya usafi wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi wananchi waendele na utaratibu huo kama ilivyopangwa ili kuendelea kutunza mazingira

Kila ifikapo june tano ya kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya mazingira ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ” mkaa gharama tumia nishati mbadala”

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search