MICHUANO YA SPORTPESA SUPER CUP LIVE NDANI YA STARTIMES

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIKA kipindi ambacho ligi zimefikia zimefikia tamati, katika king’amuzi cha StarTimes burudani bado inaendelea.

Sasa ni michuano ya SportPesa Super Cup ambayo inafanyika nchini Kenya na kushirkisha jumla ya timu nane kutoka Tanzania na Kenya.

Tanzania inawakilishwa na timu nne ambazo ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2017/18 Simba, Yanga, Singida United na JKU ambao ni mabingwa kwa Upande wa visiwani Zanzibar.

Timu hizo zinashiriki mashindano haya kwa kuwa zote ziko chini ya udhamini wa SportPesa.

Michuano hiyo imeanza kutimua vumbi tar 3 Juni itafikia tamati tar 10 Juni, na mechi zote ziko Mubashara katika kiwango cha HD kupitia king’amuzi cha StarTimes kupitia chaneli ya michezo ya Sport Focus namba 240 na ST Swahili namba 400.

“Ili mteja aweze kutazama mechi hizi atatakiwa kulipia kifurushi cha Mambo, pia anaweza kufanya malipo ya siku na akatizama mechi ambazo anazipenda”, alisema Meneja Masoko wa Kampuni ya StarTimes, Ndg David Malisa akizungumza na waandishi wa Habari.

Timu za Tanzania zinaendelea na uwakilishi wake, na mchezo wa fainali unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili na utakuwa Mubashara kupitia Sports Focus na ST Swahili ndan ya king’amuzi cha StarTimes.

Mshindi wa mchezo wa fainali atapata nafasi ya kucheza na klabu ya Everton inayoshiriki ligi Kuu ya nchini Uingereza katika dimba lao la nyumbani ST Goodison Park huko Merseyside. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search