HATIMAYA JAY DEE AWEKA WAZI 'STATUS' YAKE !!
Lady Jay D na Spicy.
WAKATI akitarajia kuzindua albamu yake ya saba Ijumaa hii, mkongwe wa Afro Pop Bongo, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amewataka wabongo kuacha kuwaziana mabaya, kwani wengi wao wanapenda wenzao waharibikiwe.
Lady Jay D.
Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa ukweli kuhusu kuachana kwake na mpenzi wake raia wa Nigeria, Spicy, kufuatia maandishi
aliyoandika katika akaunti ya mtandao wake wa Instagram, wiki tatu zilizopita, ulioashiria kuwepo kwa matatizo kwenye uhusiano wake.
“Niko vizuri na Spicy, yale maneno niliandika kwa ajili ya muziki, watu wanapenda kuona wenzao wanaharibikiwa, kwa nini wanakimbilia kuamini nina matatizo na Spicy na hawafikirii kuhusu kazi yangu? Niwakaribishe waje kwenye shoo yangu ya uzinduzi pale Lugalo Uwanja wa Gofu Ijumaa hii,” alisema Jide.
No comments:
Post a Comment