'MCHANGA WA DHAHABU' - HAPI AMPONGEZA RAIS MAGUFULI..
Sakata la makontena ya mchanga wenye Madini ambalo limegonga vichwa vya habari hivi karibuni leo limemuibua DC wa Kinondoni ambae amempongeza Rais Magufuli kwa hatua zake imara za kutetea rasilimali za taifa. Tanzania Mpya Matukio kama kawaida imefanikiwa kunasa 'exclusive coverage' kutoka kwenye official Instagram page ya DC huyo.. Fuatana nasi usipitwe na alichosema DC Ali Hapi.
919 likes
Hongera sana Mh. Rais kwa marufuku hii ya mchanga wa kutoka migodini kusafirishwa nje. Hakika kama taifa ni lazima tufike mahali tuungane kutetea rasilimali zetu kwa faida ya nchi yetu.
Sheria, mikataba na mazoea haviwezi kuwa juu ya maslahi ya taifa letu. Tuna nafasi ya kuweka sheria nzuri na kuipitia mikataba (kama ipo) na sheria (kama zipo) zinazotoa mwanya kwa rasilimali za taifa kusafirishwa kwenda nje.
Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa madini sio ndizi, kama hatutayachimba leo hayawezi kuoza (kuharibika). Kama hatuna uwezo wa kutosha kuchoma mchanga wetu nchini ili tupate madini mbalimbali ni bora tusubiri hadi tupate uwezo huo kwa faida ya taifa.
Mchanga unaotoka machimboni migodini una madini mengi ya aina tofauti na yenye thamani kubwa.
Madini haya hubainika baada ya kuchomwa kwenye kinu mchanga huo.
Hivyo kwa kuruhusu mchanga usafirishwe nje ya nchi ambako hatujui nani anayechoma, wala madini yanayopatikana baada ya uchomaji, wala thamani yake ni sawa na kuruhusu nchi kuibiwa rasilimali zake huku tukibaki na mashimo ardhini mwetu (migodini).
Tuungane kama taifa kuunga mkono juhudi hizi za Mh. Rais kutetea rasilimali zetu kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae. Hatuwezi kuwa na reli ya kisasa, barabara nzuri, elimu bora, maji safi na salama na uchumi imara kama hatutalinda rasilimali zetu.
#Tanzaniakwanza
No comments:
Post a Comment