OPERESHENI DHIDI YA MASHAMBA YA BANGI YASHIKA KASI !!

DC DANIEL CHONGOLO AONGOZA OPARESHENI YA KUTEKETEZA MASHAMBA YA BHANGI EKARI 5 WILAYANI LONGIDO

Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Longido ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Godfrey Daniel Chongolo, imeendelea na oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya Bhangi katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.

Sehemu ya Bhangi ikichomwa moto,kuhakikisha haitumiki tena kwa matumizi mengine ya ulevi.

Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Daniel Chongolo akijiandaa kuanza kuongoza oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya Bhangi akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya pamoja na DC wa wilaya ya Longido,Mh Daniel Chongol ( pichani kulia) wakiendelea na oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya bhangi katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo mkoani Arusha

Source: Michuzi Jr.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search