RC MAKALA 'AWASHA MOTO' MBEYA - ASEMA 'HAPA KAZI TUU, AWATAKA MADIWANI KUTUMIKIA WANANCHI...

 AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA MAENEO YAO



 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi mtaa wa Shewa kata ya Mwakibete mkoani Mbeya,na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kutatua Changamoto mbalimbali zinazo wakabili.

Makala ambaye ametembelea Shule ya Msingi Shewa na kushuhudia msongamano wa wanafunzi,  amepongeza wananchi kwa kushiriki ujenzi wa madarasa kupunguza msongamano wa wanafunzi, ambapo halmashauri ya jiji la Mbeya walichangia shilingi milioni 6.3 kuunga Mkono jitihada za wananchi.

Makala ameahidi kufuatilia kwa Karibu ujenzi wa madarasa mpaka yakamilike, kwani wananchi wamekuwa wakichukizwa na baadhi ya watu wachache wanaopita kushawishi wananchi wasichangie

Makala amewaonya wote wanaoshawishi wananchi kutochangia Maendeleo kuacha tabia hiyo mara moja katika  na kuamua kuonyesha mfano wa kuchangia milioni moja katika ujenzi wa choo cha Shule msingi shewa

Pia ameagiza Tanesco na Mamlaka ya Maji kushughulikia haraka matatizo ya  Umeme na Maji katika mkoa wa Mbeya hili kupunguza kero kwa Wananchi.
 Rc Makalla akizungumza na wananchi wa kata ya mwakibete jijini mbeya
Akishangazwa na wingi wa wanafunzi katika shule ya msingi mwakibete ambapo idadi ilionesha wanafunzi ni wengi kuliko madarasa.
Moja kati ya Wakazi wa shewa kata ya mwakibete wakitoa kero zao mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya.

kwa msaada wa Michuzi TV, na Fadhili Atick Globu ya Jamii Mbeya

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search