JOKATE MWENGELO NDIE KATIBU UHAMASISHAJI UVCC TAIFA; UTEUZI WAKE WAZUA SINTOFAHAMU !
Uteuzi wa Jokate Mwegelo miss Tanzania Namba 2 nyuma ya Wema Sepetu kuwa Kaimu katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa umezua sintofahamu kubwa ndani ya jumuiya hiyo. Uteuzi huo unaonekana kutaka kuivuruga jumuiyo. Mjadala mkubwa umeibuka kuhusu uteuzi huo, huku baadhi ya viongozi wa juu wa jumuiya hiyo wakidai kwamba uteuzi haukufuata kanuni na taratibu za umoja huo.
Vyanzo vya kuaminika vimedokeza kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa UVCCM hawakushirikishwa katika uteuzi huo uliofanywa kigogo mmoja wa umoja huo. "Hao wanaolalamika hawajui kanuni za UVCCM huwezi kupata nafasi kama kikao cha kamati ya Utekelezaji hakijakaa," Shaka Hamdu Shaka. JOKATE AKIZUNGUMZIA swala hilo yeye mwenye alikuwa na mtazamo chanya juu ya uteuzi wake na kuahidi kutimiza majukumu yake kwa weledi: " Nashukuru kwa imani walioonyesha viongozi wangu ila zaidi kuona nina uwezo wa kuongoza idara hiyo nyeti na muhimu kwenye jumuiya. Kikubwa ni kuifanya Jumuiya kuwa karibu na Vijana wa kitanzania na kurudisha tumaini na kuisimamia changamoto wanazozikabili vijana katika kujiletea maendeleo,"



No comments:
Post a Comment