KAMANDA SIRRO: "TUNAWASHIKILIA WATU WATATU KWA KOSA LA KUVAMIA MKUTANO WA MWENYEKITI WA CUF KINONDONI "


Na. Mwandishi wetu - Matukio
Kamishina wa kanda maalumu ya Dar Es Salaam Simon Siro amesema mapaka sasa watu watatu wanashikiliwa kuhusiana na tukio la kuvamiwa kwa mkutano wa Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) wilaya ya kinondoni siku ya Jumamosi  ya wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatatu) Siro amesema shauri la kesi hiyo limekwishafunguliwa na upelelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika huku akitoa rai kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaotoa vitisho kuwa watawafuata watu flani ili kuwashughulikia.
“Hakuna mtu au kikundi cha watu wanaweza kuwa na mamlaka ya kuwashambulia wenzake mtu kama ana malalamiko yake anapaswa kuyapeleka mahakamani na kama ni ya jinai ayapeleke polisi lakini sio kuwavamia watu kama vile wewe upo juu ya sheria,”alisema Siro.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search