"NATAKA KUISUKA UPYA YANGA IFIKE MBALI AFRIKA" - YUSUFU MANJI


Manji amewataka mashabiki wa timu hiyo kutosononeka sana kwa kipigo cha mabao 4-0 na kutolewa kwenye michuano ya kimataifa na MC Alger

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutosononeka sana kwa kipigo cha mabao 4-0 na kutolewa kwenye michuano ya kimataifa na MC Alger kani kuna jambo zuri ameliandaa kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Manji ameiambia Goal, anachotaka ni kuhakikisha timu hiyo inapambana kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani kwa kubeba taji la ligi ya Vodacom au ubingwa wa kombe la FA na baada ya hapo atafanya mambo makubwa okowepo kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa watakaoipa mafanikio makubwa timu hiyo.

"Niliongea na timu kabla ya kwenda Algeria lakini pia niwaambie mashabiki wetu hawapaswi kukata tamaa ni kweli tumetolewa lakini tuendelee kuipa sapoti timu yetu ili iweze kupata nafasi nyingine ya michuano ya kimataifa nataka kuisuka upya Yanga ili iwe na uwezo wa kucheza mashindano makubwa Afrika na kufika mbali," amesema Manji.

Kiongozi huyo amesema kilichosababisha timu kuyumba ni matatizo aliyopata, lakini ingawa bado hayamalizika anaamini yatakaa sawa nakutimiza lengo lake la kukiimarisha kikosi hicho kwa kumruhusu kocha Lwandamina kusajili mchezaji anayemuhitaji.

Amesema hilo kwake halina tatizo isipokuwa amemtaka kila mmoja kutimiza majukumu yake ndani ya timu na kuifikisha pale walipokusudia ingawa wana matatizo ya mishahara kwa kipindi hiki cha matatizo.

Amesema Yanga ni timu kubwa Afrika na kama Mwebgekiti hatokubali kuona wanahadhirika kwa kushuka chini kimafanikio ndiyo maana anataka kurudisha ubora wa timu ili kufikia kile walichokikusudia msimu huu.

Kipigo cha jana kimeifanya Yanga kutolewa kwenye mochuano ya Kombe la shirikisho Afrika, kwa jumla ya mabao 4-1 na sasa inarejea nyumbani kuhakikisha inatafuta nafasi nyingine ya lushiriki michuano hiyo ambayo haijawahi kukosa kwa kipindi cha miaka 26 mfululizo.

Source: SS.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search