VIDEO: NAPE ATOLEA UFAFANUZI KITENDO CHA KUPITA JUU YA MIGONGO YA WAMAMA

Mbunge wa Matama, Nape Nnauye ametolea ufafanuzi picha zake zilizosambaa zikimuonyesha akipita juu ya wanawake waliolala chini na kusema kuwa hiyo ni moja ya mila za kwao.
Source: swahili times

Nape ameyasema hayo baada ya picha hizo kuzua mvutano mkubwa ambapo amesema kuwa, kitendo kile ni sehemu ya mila za kwao ambapo hufanywa kwa mtu ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuheshimika sana.
Amesema yeye mwenyewe awali alikataa kupita juu ya migongo ya wanawake hao, lakini wenyewe walimlazimisha na kumwambia, kama asingepita ingekuwa ni dharau kubwa sana ameonyesha kwao.
Nape ameyasema hayo leo wakati wa mkutano na wazee wa Jimbo la Mtama aliokutana nao leo kutoa shukrani zake kufuatia mapokezi makubwa aliyoyapokea jana alipofika kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Kiwalala, Jimbo la Mtama, Wilaya ya Lindi Vijijini mkoani Lindi.
Hapa chini ni video ya Mbunge Nape Nnauye akitolea ufafanuzi tukio hilo.



No comments:
Post a Comment