VIDEO: Wakili Kambole amezungumzia kuhusu Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki

April 2 2017, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya uchaguzi wa Wabunge watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Afrika Mashariki ambao walihitajika Wabunge Tisa.
Baada ya uchaguzi huo, ni wabunge saba; wabunge sita kutoka CCM na mmoja CUF wamepatikana huku wabunge wawili wa CHADEMA wakipigiwa kura ya hapana hivyo kufanya kuwa na pengo la Wabunge wawili ili kukamilisha idadi inayotakiwa kwa mujibu wa Mkataba wa Afrika Mashariki unaozitaka kila nchi mwanachama Wabunge Tisa.
Leo April 8, 2017 Ayo TV na millardayo.com ilimtafuta Wakili wa kujitegemea Jebla Kambole ambaye pia ni Mwanasheria wa Haki za Binadamu Tanzania ili kufafanua kitu gani kitaendelea baada ya tukio hilo na iwapo Wabunge hao saba wataapisha ili kuendelea na shughuli za EALA.
“Kanuni zinaelekeza kwamba, upige kura za tiki kwa watu tisa, halafu ukaweka tiki kwingine ukaweka kosa. Je, hiyo kura itakuwa halali au siyo halali? Ni miongoni mwa changamoto za kisheria ambazo zimejitokeza katika uchaguzi huu…” – Jeba Kambole.
Hapa Wakili Kambole anafafanua…

VIDEO: Matokeo ya wabung

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search