Mama Samia kuongoza shughuli za kuaga miili ya Wanafunzi waliofariki kajika ajali ya basi juzi.



Makamu w a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo  mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo  Mhe. Makamu wa Rais ataongoza  wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kuaga miili ya wanafunzi,na waalimu waliofariki kwenye ajali ya gari. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
AU2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha jioni hii ambapo hapo kesho ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali jana tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule  iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.
Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hapo kesho.
Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo - jamiiblog

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search