10 News !! Maalim Seif 'atema cheche' asema si Lipumba.. bali ni Mungu tu ndie anaeweza kuzuia haki isipatikane.. #share.. BASATA nao wamkana Ray Vanny !!

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim seif Sharif Hamad, amefunguka mengi yanayokihusu chama na mustakabali wake kufuatia maamuzi ya RITA ya hivi karibuni ya kuitambua rasmi Bodi ya chama cha CUF iliyo chini ya Profesa Lipumba.

Akiongea na Waandishi wa Habari Mchana huu Jijini Dar es Salaam, Maalim amesema mambo yote yanayojitokeza yana majibu ya kisheria, na chama chake hususan kambi iliyo chini yake imejiandaa kuyamaliza kwa njia za Kimahakama, na kwamba kwa hatua walizozifikia ni Mwenyezi Mungu tu ndio anaeweza kuzuia haki isipatikane na si Lipumba na genge lake!!

Chama chama CUF kimeingia kwenye Mtafaruku mkubwa kufuatia maamuzi ya Lipumba kujiuzulu kwa hiari na kisha kurudia nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama kufuatia 'kwenda fyongo' kwa Mikakati, na Matokeo mabaya ya chama chao katika uchaguzi uliopita..

Akifafanua zaidi Maalim alisema, kwa katiba na misingi ya chama anaamini bodi ya ni feki kwa vile mamlaka kamili ya uteuzi wa Baraza hilo yapo chini ya mamlaka ya Baraza Kuu, na si chini ya Lipumba ambae licha ya kuwa si Mwenyekiti wa CUF, lakini pia si mwananchama wa chama hicho.













About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search