Qatar Yaapa kutosalimu amri kwa Saudia.. #share 'vikwazo hivi ni kinyume na mahusiano ya kimataifa..'
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Qatar amewalaumu majirani wake wa Ghuba, kwa kukataa mazungumzo kuhusu matakwa yao, ili kurejesha safari za ndege, baharini na ardhini kwa taifa hilo. Sheikh Mohammed Al Thani alisema kuwa hatua hizo ni kimyume na mahusiano ya kimataifa.
Saudi Arabia, Milki ya nchi za kiarabu, Bahrain na Misri, wanaishutumu Qatar kwa kuunga mkono Ugaidi, na zimeipa masharti kadha ambayo waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Saudi Arabia ameyataja kuwa yasiyo jadiliwa
Hatua ya kuitenga Qatar imezua wasi wa wasi chini Qatar, nchi yenye utajiri wa mafuta na gesi inayotegemea ununuzi wa bidhha kutoka nje kwa watu wake milioni 2.7
Siku ya Ijumaa mataifa hayo manne ya kiarabu yaliipa Qatar orodha ya masharti 13 inayotakiwa iyatimize ili kumaliza mzozo ikiwemo ya kukifunga kituo cha Al Jazeera, kufunga kambi ya jesho la Uturuki, kukata uhusiano na kundi la Muslim Brotherhood na kulegeza uhusiano na Iran
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson, ambaye amejitolea kumaliza mzozo huo amesema kuwa baadhi ya masharti ni magumu kuyatimiza, lakini kuna mengine ambayo yatahitaji mazungumzo.
Lakini baada ya kufanya mazungunzo na bwana Tillerson mjini Washington, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa saudi, alipokuwa akiulizwa ikiwa matakwa yatajadaliwa alijibu kuwa hayatajadiliwa - BBC swahili
No comments:
Post a Comment