ACT Wazalendo yakemea Jeshi la Polisi.. #share.. ' haiwezekani muwapige na kuwaswaga Watu wenye Ulemavu.. tunalaani.."

Dar es Salaam. Chama cha ACT-Wazalendo kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwazuia kwa nguvu walemavu waliotaka kwenda kumuona Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Ilala.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Juni 18), Katibu wa Itikadi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema walemavu hao walikusanyika ili kwenda kupeleka malalamiko yao dhidi ya askari wa usalama barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katikati ya Jiji.
"Juni 16 askari wa polisi waliwavamia, kuwapiga, kuwaswaga na kuwaburuza watu wenye ulemavu," amesema Shaibu.
ACT imemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuomba radhi kwa jumuiya ya watu wenye ulemavu nchini na kuhakikisha vitendo hivyo havirudiwi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search