Video: Maandamano kila kona Jijini London.. #share.. 'tunataka Ripoti ya Grenfell.." Waziri mkuu awekwa kikaangoni!!!
Kauli ya Idara inayohusika na Majanga ya Moto Nchini Uingereza ya kwamba ripoti ya Moto wa Grenfell haitawekwa hadharani imeamsha hasira za wananchi ambao wameamua kuingia mitaani kuandamana kudai uwazi na ukweli katika kuliendea tukio la Grenfell.
Kumekuwa na shakashaka nyingi juu ya sababu hasa zilizopelekea jengo la hilo kubwa lenye makazi ya familia 120 kuungua, lakini shaka zaidi ni tabia ya moto huo, spidi na njia (sweeping fire) iliyofanya waliomo ndani kushindwa kujiokoa kinyume na taratibu za kawaida na kanuni za uokoaji(fire rescue procedures).
Katika hali iliyoonekana kucheza 'karata' ya kisiasa, Meya London Mstahiki Sadiq Khan jana alimuandikia barua ya wazi Waziri Mkuu Theresa May akimtaka aviagize vikosi vyake viharakishe kuchapisha ripoti hiyo kwani Waingereza wana kiu ya majibu..
Mapema jana mamia kwa maelfu ya raia waliobeba mabango ya kuilaumu Serikali kwa jinsi ilivyojivuta kushughulikia janga la Grenfell, walikusanyika mitaa maarufu ya Oxford na Notigham wakipiga mayowe ya kuonyesha mshikamano kwa familia zilizoathiriwa na ambazo zimetapakaa bila msaada..
Kwengineko vyama vikuu vya upinzani vimechagiza juhudi za Bi Maya anaetarajiwa kuunda Serikali ya mseto na wametishia kutomuunga mkono kutokana na jinsi alivyoshughulikia suala la Grenfell na suala la Uingereza kujitoa Sarafu ya Euro.

No comments:
Post a Comment