Breaking News!! mirindimo mikali yahamisha kijiji Kibiti.. #share

Hali ya taharuki imewakumba wakazi wa vitongoji vya Vitongoji vya Msogole na Mkata  vilivyopo wilayani Kibiti, na kusabababisha kuyakimbia makazi yao kutokana kukithiriri kwa mirindimo mizito ya silaha zinazosadikiwa kuwa risasi.


Milio hiyo iliyoanza kusikika mida ya saa nane usiku ilisababisha wananchi kujigawa katika makundi makundi na kuanza kukimbia ambapo baadhi ya wananchi wengine walikimbilia katika kijiji cha Mtunda na maeneo mengine alidokeza Bw. Khalid toka kijiji cha Mkata.

Alisema kutokana na milio hiyo kuwa mizito na mingi wakazi wa vitongoji hivyo walianza kukimbia ovyo kwa kuwa haikutambulika ni akina nani waliokuwa wakiipiga.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Mchukwi Ami Ngaruka alisema amepokea wananchi 14 toka katika kitongoji cha Msogole na Mkata vilivyopo katika kijiji cha Muyuyu kwa madai wanakimbia milio ya silaha zilizokuwa zikipigwa toka katika Msitu wa Mbunguluni.

Hata hivyo, kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Onesmo Lyanga amesema hajawa na taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search