Good News!! Mama Janet Magufuli atoa 'afueni' kwa kwa yatima !


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na viongozi wa vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kabla ya kuwakabidhi vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017.


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Hajat Mwanaisha Magambo mkuu wa kituo cha New Life Orphanage cha Boko Dawasco kwa niaba ya viongozi wa vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu waliopewa vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017. Vituo vilivyopkea vyakula hivyo ni pamoja na New Life kilichopo Boko Dawasco chanye watoto 121, Charambe Islamic kilichopo Charambe (watoto 54), Mwandaliwa Centre kilichopo Mbweni (watoto 94) Al Madina Children Home cha Tandale ( watoto 65), Ijangozaidia Orphanage Centre kilichopo Sinza (watoto 1030, Azam Orphanage kilichopo Mbagala (watoto 51), Hiari Orphanage kilichopo Chang’ombe (watoto41) na CHAKUWAMA (watoto 64) kilichipo Sinza.



Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsabahi mmoja wa yatima maaba ya kumkabidhi vyakula Hajat Mwanaisha Magambo kutoka kituo cha New Life Orphanage cha Boko Dawasco kwa niaba ya viongozi wa vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu waliopewa vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017

PICHA NA IKULU

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search