Count Down ! Mbivu Mbichi ya Joshua Nassary Bungeni yamsubiri Mkuchika leo.. #share

Kamati ya Kudumu ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge chini ya Mwenyekiti wake Mhe. George Mkuchika, leo inatarajiwa kuwasilisha Ripoti Maalum ya Kiuchunguzi kuhusiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasary kudharau Mamlaka ya Spika.



Macho na masikio ya wananchi wengi yako Dodoma kufuatia makali yaliyoonyeshwa na Kamati hiyo iliyompa Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Esther Bulaya vifungo vya mwaka mmoja mmoja nje ya Vikao vya Bunge kufuatia sakata la Mnyika..

Ripoti ya leo ya Mhe. Mkuchika pia inatarajiwa kumgusa Mhe. Concesta Rwamlaza (Viti Maalum Chadema).

Ungana nasi kupitia channel ya Bunge stream baada ya kikao kinachoendelea cha maswali na majibu kupata yatakayojiri wakati wa uwasilishaji wa Ripoti hiyo maalum.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search