Good news!! NASA waja na Ndege ya 'Mwendokasi' itakimbia zaidi ya mwendo wa Sauti ikiwa angani... #share

Shirika la Ndege la Usafiri wa Anga za juu la Marekani (NASA) linatarajia kujikita kwenye usafiri wa Ndege za abiria na hivi karibuni itazindua Ndege yake ya kwanza yenye Speed ya Supersonic.



Vyanzo vya habari vya ndani shirika la NASA vimesema ndege hiyo itakayotumia Teknolojia  ya kisasa zaidi ya QSST(Quiety SuperSonic Transport) itakuwa na uwezo wa kuruka bila kutoa sauti (disruptive sonic boom) na itakuwa na uwezo kukimbia zaidi ya sauti iwapo angani.
Taarifa za ubunifu huo zimekuja kufuatia kudoda kwa biashara ya ndege yenye sifa kama hizo ya Concord na wamiliki wake kuamua kuiondoa sokoni miaka 10 iliyopita.
Mbunifu wa Ndege hiyo Lockheed Martin, amepasha habari kwamba kazi ya ubunifu wa muonekano wa Ndege yao mpya tayari umekamilika.. na itaanza safari yake ya kwanza ya abiria mwaka 2021.. 
"kwa sasa kila kitu kimekamilika, kinachoendelea ni kutengeneza ndege ndogo (a single seated aircraft) kwa ajili ya majaribio ya awali na ya mwisho..." aliongeza Eng. Martin..

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search