Tetesi za usajili ! Ngoma Kutumika Yanga Miaka Miwili.. #share.. Kapombe + Okwi = Mafisango !!

Mshambuliaji nguli wa Timu ya Soka ya Yanga, Donaldo Dompo Ngoma, ametegua kitendawili kilichokuwa kimewazonga mashabiki wake kwa kurejea klabuni hapo na kuongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu.

Wakati huo huo.. Beki mpya wa Simba, Shomari Kapombe amesema kurejea kwao akiwemo Emmanuel Okwi ni sawa na kuirejesha Simba ya enzi za Patrick Mafisango.

Kapombe ambaye amerejea Simba akitokea Azam FC, amesema amefurahi kwa kuwa anaamini kikosi chao kitakuwa imara na kinachotakiwa ni ushirikiano tu.

Mafisango alikuwa kiungo wa Simba raia wa DR Congo na alifariki kwa ajali ya gari mwaka 2012. 
“Itakuwa ni sawa na Simba ya kipindi cha kina Mafisango, wanaweza kuongeza nguvu tu katika ulinzi zaidi.

“Lakini hii itakuwa ni Simba yenye ushindani mkubwa na kama tutashirikiana na kujituma, ninaamini tutafanya vizuri,” alisema.






About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search