Habari mpya za hivi punde: Wahalifu wamewajeruhi watu wawili kwa Risasi na kisha kuondoka na majeruhi hao..

 Taarifa mpya zilizotufikia hivi punde kutoka mkoa wa Pwani zinasema, taarifa kutoka Jeshi la pilisi mkoa huo ni kwamba wahalifu wamewapiga risasi watu wawili kisha kuondoka na majeruhi hao... amethibitisha Kamanda wa Polisi Mkoa RPC Onesmo Lyanga.

Tunaendelea kufuatilia taarifa hizi usikae mbali kupitia..  www.matukiotza.blogspot.com

=========================================================
Mapema leo asubuhi Blog yako ya Matukio iliripoti uwepo wa vifo vya watu watatu kwenye tukio hilo.
__________________________________________________________
Kuna Taarifa ya kusikitisha tumeipokea hivi punde ambapo watu watatu wakazi wa Kijiji cha Nyamisati katika kata ya Salale wilayani Kibiti wanasadikiwa kufariki dunia kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Leo.

Mkazi mmoja wa Kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina  moja la Hamza amesema miongoni mwa watu waliopigwa yumo mwanamke mmoja ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji kimojawapo kijijini hapo.

Watu hao wanaosadikiwa kupoteza maisha ni Hamid Kidevu,Yahaya Mkame na Moshi Machela.

Mkuu wa wilaya ya Kibiti Gullamuhusein Kifu amesema ameliagiza jeshi la Polisi wilaya hapa kwenda eneo hilo kwa ajili ya uthibitisho.

Matukio blog tunaendelea kukupasha yatakayojiri baada ya taarifa ya Jeshi la Polisi.

Source- Mcl digital

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search