Video: Zitto apigigilia 'msumari wa mwisho' kuvuliwa Uenyekiti mama Anna Mghwira.. #SHARE asisitiza ni busara imetumika !

Kiongozi Mkuu wa chama cha upinzani ACT Wazalendo Mhe. Zitto Luyaga Zubari Kabwe, ametoa msimamo mkali wa chama chake juu ya kumpumzisha mama Anna Mgwira nafasi yake ya uenyekiti katika chama, baada ya kuteuliwa na chama kilichoko madarakani kuwatumikia wananchi kwenye ofisi ya umma kama Mkuu mpya wa Mkoa Kilimanjaro.

Akiongea kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri kupitia chama chake, alibainisha wazi kuwa katiba ya ACT haikuwa na kipengele kinachoweka bayana muongozo wa ushirikiano wa ACT na chama chengine katika kuendesha Serikali. 

Katika kulitambua hilo Baraza Kuu la Uongozi la chama chake, limetumia busara kumpumzisha mama Mghwira ili aweze kutumikia nafasi yake mpya kwa ufanisi, na kwa manufaa ya wananchi wa Kilimanjaro, na kuitetea, kuilinda na kuitekeleza vyema Ilani ya uchaguzi ya chama kilichomteua kama alivyoahidi wakati anakula kiapo.

Itakumbukwa ni hivi majuzi tu mama Mghwira alikinzana na msimamo wa baraza hilo, na kwamba yeye bado ni mwenyekuti halali wa ACT Wazalendo !

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search